Mke wa Mtu Ajiumiza Baada ya Kumfumania Mume mumewe Akijinafasi na msichana wa kazi
Adili Tende at 8:20 AM
UBABE! Tofauti na inavyoaminika na wengi kuwa mfumaniwaji huwa mpole,
kibao kimebadilika, mfanyakazi wa ndani aliyejulikana kwa jina la
Niachie amegeuka mbogo na kumchoma bisibisi bosi wake, Amina ‘Mama Zai’
aliyemfumania akiwa na mumewe aitwaye Amri.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Mbagala jijini Dar ambako mama
Zai alimwekea mtego mfanyakazi wake huyo wa ndani baada ya kubaini kuwa
alikuwa akiwa a na mumewe wakati yeye akiwa kazini.
Akizungumza na paparazi wa kitengo maalum cha kufichua maovu () siku
mbili kabla ya tukio, mama Zai alidai kuwa mumewe ana kawaida ya kufanya
mapenzi na mfanyakazi wao wa ndani wakati yeye akiwa kazini hivyo
akaandaa mtego ili kukomesha tabia hiyo.
Mama Zai alizidi kumwaga data kuwa, yeye ni nesi katika hospitali moja
ya mtu binafsi iliyoko Jangwani jijini Dar hivyo akiwa zamu ya usiku,
mumewe hutumia mwanya huo kubanjuka na hausigeli.
“Ananivizia nikitoka tu na akijua nimeshafika mbali, anaingia chumbani
kwa hausigeli na kuvunja naye amri ya saba,” alidai mama huyo.
Mama huyo alisema ili kufanikisha zoezi la kumnasa mumewe, alijifanya
anakwenda zamu ya usiku kisha akajifungia stoo ili aweze kufanya
fumanizi matata.
kama kawaida tulitia timu timu nyumbani kwa mama huyo ikiwa kamili na zana
zake, ikakita kambi katika baa moja iliyo jirani na nyumba hiyo na
ilipofika saa tano usiku, ishu ikatiki, baba Zai aliingia katika chumba
cha mfanyakazi huyo kwa lengo la ‘kuharibu
Katika harakati za kujinasua katika kipigo cha bosi wake, hausigeli huyo
aliokota bisibisi na kumchoma mama mwenye nyumba shingoni kisha kutimua
mbio huku mume naye akiingia mitini.

No comments:
Post a Comment