Sunday, June 1, 2014

Matumizi ya ARV, pombe yanavyohatarisha maisha

Share bookmark Print Email Rating
Pombe 
Na Adili Tende

Posted  june1  2014  saa 06:18 AM
Kwa ufupi
Madhara yanayoweza kujitokeza kwa kutumia ARV na pombe ni kukojoa mara kwa mara, endapo amekunywa ARV basi haziwezi kufanya kazi
SHARE THIS STORY
0
Share


Dar es Salaam. Watu wanaokunywa dawa za kufubaza makali ya Virusi Vya Ukimwi(ARV) huku wakitumia pombe kwa wingi wametajwa kujiweka katika hatari zaidi.
Wanaweza kuharibu dozi na kusababisha kushuka kwa kinga ya mwili, kuongeza kiwango cha sumu mwilini, kuharibu ini na figo.
Watalaamu wa afya wanasema kuwa kiasi kidogo cha pombe kwa mtu anayeishi na VVU, hakina madhara jambo ambalo pengine limesababisha watumiaji wengi wa ARV kubobea katika ulevi na kuhatarisha afya zao.
Mtafiti wa Masuala ya Ukimwi, Kutoka Taasisi ya Utafiti wa Tiba nchini, NIMR, Dk Edward Maswanya anasema hairuhusiwi hata kidogo kuchanganya pombe na dawa, kwani pombe huua nguvu ya dawa.
Anasema pombe inasababisha usugu wa dawa hali ambayo huchangia dawa hizo zisifanye kazi yake inavyotakiwa.
“Sioni umuhimu wa mtu anayetumia ARV kunywa pombe, anajiua mwenyewe kwa sababu anasababisha usugu wa dawa na anaweza kupata mabadiliko makubwa kwenye mwili yatakayomuathiri,”anasema.
Utafiti mwingine uliochapishwa na Jarida la Tiba la Boston, 2013 uligundua kuwa karibu nusu watu wanaoishi na VVU na ambao wanatumia ARV, huacha kutumia dawa baada ya kulewa sana na kuharibu ratiba ya dozi zao.
Kwa kufanya hivyo utafiti huo uligundua kuwa wanaharibu kiwango chao cha kinga(CD4).
Katika utafiti huo, watafiti walitumia sampuli ya watu 178 wanaokunywa pombe na kutumia ARV, na kuwafuatilia kwa miezi 12.
Walibaini kuwa mtu mmoja kati ya wanne, aliacha kutumia dawa jambo lililochangia kushuka kwa kinga ya mwili.
“Asilimia 51 ya watumiaji wa pombe wanaotumia ARV, walichangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kinga ya mwili hadi CD4 chini ya 200,” unasema utafiti huo.
Mfamasia katika Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa (CDC) cha jijini Dar es Salaam, Charles Lymo anasema watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi, wana kipimo maalum cha kunywa pombe ambacho hakitakiwi kuzidi lita 1.6.

No comments:

Post a Comment