Friday, June 6, 2014

Sintah Ampa Pole Capt. Komba Kwa kudharilishwa

"Kwakweli watu wakikuamulia wamekuamulia aisee, picha hizi ni za uzushi na zimetengenezwa wabataka kumchafua Mh Komba, hivi uko chumbani na baby wake wewe uvae khabga yeye awe na shirt badala ya vest kama kweli mko wenyewe kimahaba? Khaa eti na mabusu juu inamaana Mh alikuwa anaona picha zinapigwa na yeye akauchuna?? maana ni picha za kujiandaa haswa 

Mchumba wa Kwanza wa Flora Mbasha Afunguka, Kumbe Nae Alibambikiziwa Skendo

Flora Mbasha alikuwa na mchumba anaitwa Imma Lushanga Ambae Baba yake ni Mmiliki wa Mabasi ya Lushanga huko Mwanza kabla hajaja Dar akiwa amechumbiwa tayari Wiki mbili kabla ya kufunga ndoa Flora akapata safari ya kwenda UK ambako wenyeji wake walimshauri kwamba kwa uzuri wake atapata Mume mzungu mwenye pesa kuliko Imma yule wa Mwanza. Ili kumkimbia Imma Flora na familia yake wakamtengenezea ishu Imma mchumba wake kwamba ana Ukimwi kwa hiyo Flora hawezi kuolewa naye, Hii Nakumbuka ilikuwa Stori kubwa Sana Mwanza Kipindi Hicho zaidi ya Miaka kama Kumi na nne iliyopita mpaka leo Imma hajawahi kuoa tena na wala hana hamu 

Mke wa Mtu Ajiumiza Baada ya Kumfumania Mume mumewe Akijinafasi  na msichana wa kazi

UBABE! Tofauti na inavyoaminika na wengi kuwa mfumaniwaji huwa mpole, kibao kimebadilika, mfanyakazi wa ndani aliyejulikana kwa jina la Niachie amegeuka mbogo na kumchoma bisibisi bosi wake, Amina ‘Mama Zai’ aliyemfumania akiwa na mumewe aitwaye Amri.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Mbagala jijini Dar ambako mama Zai alimwekea mtego mfanyakazi wake huyo wa ndani baada ya kubaini kuwa alikuwa akiwa a na mumewe wakati yeye akiwa kazini.
Akizungumza na paparazi wa kitengo maalum cha kufichua maovu () siku mbili kabla ya tukio, mama Zai alidai kuwa mumewe ana kawaida ya kufanya mapenzi na mfanyakazi wao wa ndani wakati yeye akiwa kazini hivyo akaandaa mtego ili kukomesha tabia hiyo.
Mama Zai alizidi kumwaga data kuwa, yeye ni nesi katika hospitali moja ya mtu binafsi iliyoko Jangwani jijini Dar hivyo akiwa zamu ya usiku, mumewe hutumia mwanya huo kubanjuka na hausigeli.
“Ananivizia nikitoka tu na akijua nimeshafika mbali, anaingia chumbani kwa hausigeli na kuvunja naye amri ya saba,” alidai mama huyo.
Mama huyo alisema ili kufanikisha zoezi la kumnasa mumewe, alijifanya anakwenda zamu ya usiku kisha akajifungia stoo ili aweze kufanya fumanizi matata.
  kama kawaida tulitia timu  timu nyumbani kwa mama huyo ikiwa kamili na zana zake, ikakita kambi katika baa moja iliyo jirani na nyumba hiyo na ilipofika saa tano usiku, ishu ikatiki, baba Zai aliingia katika chumba cha mfanyakazi huyo kwa lengo la ‘kuharibu
Katika harakati za kujinasua katika kipigo cha bosi wake, hausigeli huyo aliokota bisibisi na kumchoma mama mwenye nyumba shingoni kisha kutimua mbio huku mume naye akiingia mitini.

Jamani Huyu Halima Kimwana ni Nani Kwa mtu Diamond?

Kuna watu wanashangaza kidogo,siyo kwamba tunawafuata majumbani mwao na kugundua tabia zao,kwamba wanakula sana,wachoyo,wachafu au hawapatani na majirani zao,hapana,wanayoyafanya ama kuzungumza,wanatufanya tuwatambue.Lakini tunaishia kuwajua kwa majina na matukio yao.Ukiniuliza babu Tale ni nani,fasta nitakujibu kuwa ni msaidizi wa shughuli za Diamond,Romie Jones nitakuambia ni ndugu yake Diamond,Wema Sepetu,ni usingizi wa Diamond,kwa maana ya mpenzi,lakini ukiniuliza Halima Kimwana ni nani,naweza kulipuuzia swali lako kwa maana sitambui wala kujua ni nani kwa Diamond.
Siwezi kuacha kujiuliza hivi huyu binti wa mjini  ni nani kwa Diamond?rafiki,dada,shemeji yake,mpambe au nani,Au ndiye kiunganishi chake kwa wale viumbe waliosababisha aitwe sukari ya warembo?yeye ni nani haswa hata afikie hatua ya kumchagulia Diamond mpenzi wa kuwa nae,ni nani hasa hata afikie kumaindi uwepo wa Wema kwenye himaya ya Diamond,kajina kake kamezidi kukaa on ea kwa kipindi kirefu kutokana na uwepo wake karibu na Diamond,ana nguvu sana kwa Diamond,Nilipuuzia kwa muda mrefu sana nikiamini ni mtu wake wa karibu wa kumshikia poda awapo lokesheni ya video zake,au anashikilia simu zake awapo stejini,baadae nikadhani kuwa huenda ni msaidizi wa mambo binafsi ya Diamond.Lakini kufikia hatua ya kumpangia Diamond mwanamke  wa kuwa nae,kidogo hapo nashindwa kuelewa,yeye ni nani kwa Diamond?
Wadau mnaojua uhusiano wa huyu dada hebu mtujuze,ni nani,anafanya shuhuli gani,naamini wote mliosoma hii habari mna kitu..

Sunday, June 1, 2014

Kashfa saba nzito nchini

Share bookmark Print Email Rating
Rais Jakaya KIkwete 
Na Adili  Tende

Posted  Jumapili,Juni1  2014  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini taifa kukumbwa na kashfa mbalimbali za upotevu wa fedha au kuanzisha mipango ambayo utekelezaji wake ulisababisha maumivu kwa wananchi na hakuna awamu ya uongozi wa Serikali iliyokwepa hali hiyo.
SHARE THIS STORY


Dar es Salaam. Serikali imepoteza zaidi ya Sh362.9 bilioni kutokana na baadhi ya kashfa kubwa za ufisadi na operesheni mbalimbali zilizoligharimu taifa tangu uhuru.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini taifa kukumbwa na kashfa mbalimbali za upotevu wa fedha au kuanzisha mipango ambayo utekelezaji wake ulisababisha maumivu kwa wananchi na hakuna awamu ya uongozi wa Serikali iliyokwepa hali hiyo.
Kuanzia awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere aliyeiongoza nchi toka mwaka 1961 ilipopata uhuru hadi 1986, Rais Ali Hassan Mwinyi (1986-1995), Rais Benjamin Mkapa (1995-2005) na Rais Jakaya Kikwete (2005-hadi sasa), kumeibuka kashfa mbalimbali, saba zikiwa kubwa na kulitikisa taifa.
Kashfa na operesheni saba kubwa zilizotikisa taifa ni pamoja na Operesheni Uhujumu Uchumi, ufisadi katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import Support – CIS) na Kashfa ya Rada.
Nyingine ni ufisadi Akaunti ya EPA, kashfa ya Richmond, Operesheni Tokomeza Ujangili na ile ya uchotaji mabilioni katika akaunti ya Escrow.
Operesheni Uhujumu Uchumi
Mwaka 1984 Serikali ilianzisha Operesheni Uhujumu Uchumi, iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Sokoine ili kutaifisha mali ambazo baadhi ya watu walidaiwa kujipatia kwa njia isiyo halali.
Operesheni hiyo ilishuhudia baadhi ya watuhumiwa wakimwaga fedha mitaani na majalalani, huku wengine wakitupa mali kuhofia kutiwa kwenye mkono wa sheria.
Hata hivyo, katika operesheni hiyo baadhi ya watendaji wa Serikali ambao hawakuwa waaminifu, waliitumia nafasi hiyo vibaya kutaifisha mali za baadhi ya watu, ambao hawakuwa wahujumu uchumi.
Zoezi hilo lilisababisha wananchi kadhaa hasa vijijini kuwekwa ndani na wengine kuachwa maskini baada ya kunyang’anywa mali zao ikiwamo mifugo na mashine za kusaga nafaka, kwa kudaiwa kuwa walizipata kwa njia isiyo halali.
Mfuko wa Commodity Import Support (CIS)
Miaka 24 baadaye yaani mwaka 2008, liliibuka sakata jingine lililokuwa na harufu kubwa ya ufisadi wa mabilioni katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import Support – CIS).

Matumizi ya ARV, pombe yanavyohatarisha maisha

Share bookmark Print Email Rating
Pombe 
Na Adili Tende

Posted  june1  2014  saa 06:18 AM
Kwa ufupi
Madhara yanayoweza kujitokeza kwa kutumia ARV na pombe ni kukojoa mara kwa mara, endapo amekunywa ARV basi haziwezi kufanya kazi
SHARE THIS STORY
0
Share


Dar es Salaam. Watu wanaokunywa dawa za kufubaza makali ya Virusi Vya Ukimwi(ARV) huku wakitumia pombe kwa wingi wametajwa kujiweka katika hatari zaidi.
Wanaweza kuharibu dozi na kusababisha kushuka kwa kinga ya mwili, kuongeza kiwango cha sumu mwilini, kuharibu ini na figo.
Watalaamu wa afya wanasema kuwa kiasi kidogo cha pombe kwa mtu anayeishi na VVU, hakina madhara jambo ambalo pengine limesababisha watumiaji wengi wa ARV kubobea katika ulevi na kuhatarisha afya zao.
Mtafiti wa Masuala ya Ukimwi, Kutoka Taasisi ya Utafiti wa Tiba nchini, NIMR, Dk Edward Maswanya anasema hairuhusiwi hata kidogo kuchanganya pombe na dawa, kwani pombe huua nguvu ya dawa.
Anasema pombe inasababisha usugu wa dawa hali ambayo huchangia dawa hizo zisifanye kazi yake inavyotakiwa.
“Sioni umuhimu wa mtu anayetumia ARV kunywa pombe, anajiua mwenyewe kwa sababu anasababisha usugu wa dawa na anaweza kupata mabadiliko makubwa kwenye mwili yatakayomuathiri,”anasema.
Utafiti mwingine uliochapishwa na Jarida la Tiba la Boston, 2013 uligundua kuwa karibu nusu watu wanaoishi na VVU na ambao wanatumia ARV, huacha kutumia dawa baada ya kulewa sana na kuharibu ratiba ya dozi zao.
Kwa kufanya hivyo utafiti huo uligundua kuwa wanaharibu kiwango chao cha kinga(CD4).
Katika utafiti huo, watafiti walitumia sampuli ya watu 178 wanaokunywa pombe na kutumia ARV, na kuwafuatilia kwa miezi 12.
Walibaini kuwa mtu mmoja kati ya wanne, aliacha kutumia dawa jambo lililochangia kushuka kwa kinga ya mwili.
“Asilimia 51 ya watumiaji wa pombe wanaotumia ARV, walichangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kinga ya mwili hadi CD4 chini ya 200,” unasema utafiti huo.
Mfamasia katika Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa (CDC) cha jijini Dar es Salaam, Charles Lymo anasema watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi, wana kipimo maalum cha kunywa pombe ambacho hakitakiwi kuzidi lita 1.6.