WASANII IRINGA WATOA USHAURI WA BURE KWA LULU WATAKA AOKOKE
Wakizungumza
na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wasanii hao Johari
John na Kevin Sanga walisema kuwa dhamana ya Lulu ni mapenzi ya
Mungu hivyo mbali ya kutoka mahabusu kwa dhamana bado anapaswa
kuishi kwa utulivu zaidi muda wote ikibidi kuanza kuwa karibu na
kanisa.
Hata
hivyo John alitaka waumini wa madhehebu mbali mbali kuendelea
kumwombea msanii huyo ili Mungu aendelee kusimama upande wake.
Wasanii
hao walisema kuwa suala la msanii huyo kuendekeza kujirusha kwa
sasa asilipe nafasi katika maisha yake na badala yake kumgeukia Mungu
zaidi na kuachana na mambo ambayo hayampendezi mwenyezi Mungu.